Logo Trop1 (1)

TROP ICSU in Kiswahili

ELIMU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA MTALAA WA ELIMU DUNIANI KOTE.

  1. Mabadiliko ya tabia nchi ni mojawapo wa masuala muhimu katika kipindi cha sasa.
  2. Mabadiliko haya yanaathiri maendeleo endelevu na ya kiusawa ya nchi nyingi pamoja na raia wake.
  3. Ili pawe na utatuzi wa mabadiliko ya tabia nchi, watu wanafaa wafahamishwe kuhusina na hali hii.
  4. Hatua za kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi zitahitaji utatuzi ulio na msingi wa kimaeneo lakini zinazokubalika na ulimwengu wa kisayansi.
  5. Kufungamanishwa kwa elimu ya mabadiliko ya tabia nchi katika mfumo wa elimu rasmi kutasaidia vizazi vya sasa na vile vijavyo kutambua mbinu mwafaka za kutatua, kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mradi wa TROP ICSU (https://climatescienceteaching.org/; https://tropicsu.org) unalenga kuhakikisha kuwa masomo yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi yanaingizwa katika mifumo ya elimu ya  shule za upili na vile vile vyuo vikuu. Hii itachangia utambuzi wa sababu zinazosababisah mabadiliko ya tabia nchi pamoja na madhara yake miongoni mwa wanafunzi. Mradi huu wa TROP ICSU ni kati ya maazimio ya kuhakikisha kuwa kila mwanadamu anaweza akatumia talanta, mbinu na malengo yake  katika njia inayolenga kutatua madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mradi huu unalenga kuhakikisha kuna njia za kuaminika za kufundishia masomo yanayohusu mabadiliko ya tabia nchi katika mfumo wa elimu rasmi. Hali hii itahakikisha kuwa kila mwanfunzi minghairi ya kozi anayosomea atakuwa na utambuzi wa visababishi vya mabadiliko ya tabia nchi na atakuwa na mbinu za uvumbuzi wa utatuzi wa hali hii ambayo ni ya kilimwengu.

Kutokana na hili, basi mradi wa TROP ICSU unaoana moja kwa moja na maazimio ya Umoja wa Mataifa ikiwemo azimio la nne ambalo ni elimu bora kwa wote pamoja na azimio la kumi na tatu ambalo ni mabadiliko ya tabia nchi.

Ili kuafikia malengo ya mradi huu, jopokazi la TROP ICSU lililopo katika Taasisi ya Elimu ya Sayansi na Utafiti IISER iliyopou mjini Pune imebuni na kubainisha  hazina ya vifaa kutoka sehemu mbalimbali za uliwengu. Vifaa hivi vitatumiwa na walimu kufundishia masomo maalum kwa kutumia mifano, uchunguzi, na shughuli zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi. Mradi huu umedhihirisha namna ya kufungamanisha elimu ya mabadiliko ya tabia nchi katika mtalaa uliopo. Mradi huu pia umebainisha vifaa mbali mbali vya ufundishaji kama vile (Mpango wa kazi wenye hatua zilizoelezwa kwa undani). Uwepo wa vifaa hivi ni ishara tosha ya juhudi za mradi hu kuhakikisha kuwa masomo yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi yanafungamanishwa na mtalaa rasmi wa elimu. Mradi huu pia umebainisha mbinu za ufundishaji ambazo zinaaminika kisayansi zitakazotumiwa kufundishia masomo yanayohusina na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuyafungamanisha na masomo mengine katika mtalaa. Kwa hivyo, matumizi ya vifaa vya ufundishaji vya TROP ICSU yatawasaidia walimu kufundisha elimu ya mabadiliko ya tabia nchi huku wakizingatia masomo mengine ya mtalaa.

Katika awamu ya kwanza ya mradi wa TROP ICSU, jopokazi limetoa mafunzo kupitia kwa semina kwa walimu na waelimishaji katika mataifa ya India, Bhutan, Afrika Kusini, Uganda, Misri, Ufaransa, Austria, Uchina, Uingereza na Australia. Katika semina hizi, waelimishaji walihakiki utendakazi wa vifaa hivi vya kufundishia. Wataalam wa elimu ya mabadiliko ya tabia nchi pia walihudhuria katika semina zingine na kutoa maoni yao muhimu. Ushirikiano kati ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kama UNCC: Learn, Shirika la Hali ya Hewa Duniani (W.M.O) na Shirika la Utafiti wa Tabia Nchi (WCRP) umeahakikisha kuwa, mradi wa TROP ICSU umeidhinishwa pamoja na vifaa vya kufundishia vilivyopendekezwa. Jopokazi hili pia lilipata nafsi ya kuwasilisha hatua za kielimu walizopiga katika 4th UN STI Forum 2019 tarehe 15/05/2019 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa yaliyoko New York na vile vile katika High Level Political Forum on Sustainable Development 2019 (HLPF 2019) katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 11/07/2019 chini ya mada “Practices and Approaches on quality education towards environment and climate action”. Vile vile, jopokazi hili limeshiriki katika mafunzo ya tabia nchi mjini COP 24 huko Uholanzi na pia semina zinazoandaliwa na walemishaji wa tabia nchi pamoja na walimu.

Mradi wa TROP ICSU ni wa kisasa na unaangazia masuala ibuka miongoni mwa vijana pamoja na juhudi za nchi kama Italia kuhakikisha kuwa, elimu ya tabia nchi inafungamanishwa katika mtalaa wa elimu.

Awamu ya kwanza ya mradi wa TROP ICSU ilipata ufadhili wa miaka mitatu kutoka kwas International Science Council (ISC).

SUBSCRIBE

To Subscribe to our newsletter please enter